Bendera ya Honduras
Mandhari
Bendera ya Honduras ina milia mitatu ya kulala yenye rangi za buluu-nyeupe-buluu. Katikati kwenye mlia mwekundu kuna nyota tano za buluu.
Bendera jinsi ilivyo imepatikana tangu mwaka 1866. Asili yake ni bendera ya "Shirikisho la majimbo ya Amerika ya Kati" kati ya 1823 na 1838.
Nyota tano hukumbusha nchi tano zilizoungaishwa katika shirikisho hili kwa matumaini ya kwamba umoja utarudishwa siku moja tena.