Bazedoksifini
Bazedoksifini, yaani Bazedoxifene, inayouzwa kwa jina la chapa Conbriza ni dawa inayotumika kutibu hali ambayo mifupa inakuwa dhaifu na mgumu baada ya kukoma hedhi.[1] Inapunguza hatari ya kuvunjika kwa uti wa mgongo lakini si kuvunjika kwa nyonga. [1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na hisia ya ghafla ya joto kali zaidi kwenye uso, shingo na kifua na jasho jingi, mkazo wa misuli, na uvimbe wa miguu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuganda kwa damu.[1] Dawa hii haipaswi kutumiwa wakati wa ujauzito.[1] Ni kidhibiti cha kipokezi cha estrojeni kilichochaguliwa (SERM).[1]
Bazedoksifini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu huko Uropa mnamo mwaka wa 2009.[1] Nchini Marekani, inapatikana kwa kuchanganya tu kama estrojeni ya bazedoxifene/conjugated.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Conbriza". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Selective Estrogen Receptor Modulators". LiverTox: Clinical and Research Information on Drug-Induced Liver Injury. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bazedoksifini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |