Bat Conservation International

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bat Conservation International (BCI) ni shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na kuhifadhi popo na mazalia yake kwa kutumia mbinu za usimamizi wa wanyama pori,kutoa elimu na kufanya tafiti mbali mbali.

BCI ilianzishwa mwaka 1982 na mwanabiolojia wa popo ndugu Merlin Tuttle, ambaye aliongoza shirika hili mpaka alipostaafu mwaka 2009.[1] Tangu kuanzishwa kwake BCI imefanikiwa kushirikiana na U.S. Fish na Wildlife Service pamoja na mawakala wengi pamoja na mashirika yasiyo ya kutengeneza faida ya kitaifa na kimataifa na limefanikiwa kuzalisha machapisho, warsha, masomo, tafifiti na miradi Marekani na Kimataifa. BCI imeajiri wafanyakazi ambao ni wanabiolojia ,wafundishaji na wasimamizi 30 na ina wanachama ndani ya nchi 60 duniani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The Founder Passes the Baton". Bat Conservation International (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-22. Iliwekwa mnamo 2021-08-23.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)