Azilsartan
Azilsartan, inayouzwa kwa jina la chapa Edarbi, ni dawa inayotumika kutibu shinikizo la juu la damu.[1][2] Matumizi yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa kisukari wa figo na kushindwa kwa moyo.[3] Dawa hii inachukuliwa kwa njia ya mdomo.[3] Kwa ujumla, athari zake hutokea ndani ya wiki mbili.[3]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara na kizunguzungu.[1][2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uvimbe usio na uchungu chini ya ngozi unaosababishwa na mzio (angioedema), shinikizo la chini la damu na matatizo ya figo.[3] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[4] Dawa hii ni kizuizi cha vipokezi vya angiotensin II.[1]
Azilsartan iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2011.[1][2] Nchini Uingereza, wiki 4 hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) chini ya £20 kufikia mwaka wa 2021.[5] Kiasi hiki nchini Marekani ni kama dola 160.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Edarbi- azilsartan kamedoxomil tablet". DailyMed. 26 Julai 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Februari 2019. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Edarbi EPAR". European Medicines Agency (EMA). 18 Mei 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "Azilsartan Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Azilsartan medoxomil (Edarbi) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 17 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 189. ISBN 978-0857114105.
- ↑ "Azilsartan Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 17 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Azilsartan kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |