Artur Aleksanyan
Mandhari
Artur Aleksanyan (amezaliwa 21 Oktoba 1991) ni mcheza mieleka katika mtindo wa Greco-Roman kutoka Armenia. Ni bingwa wa Michezo ya Olimpiki (2016), ni mshindi wa medali ya fedha (2021), ni mshindi wa medali ya shaba (2012), ni bingwa wa dunia mara tatu (2014, 2015, 2017) na ni bingwa wa mashindano ya Uropa kwa mara tano (2012, 2013, 2014, 2018, 2020). Aleksanyan ndiye mshindi wa pili wa medali ya dhahabu ya Michezo ya Olimpiki nchini Armenia tangu kupata uhuru wake mnamo mwaka 1991.Amepewa jina la utani "Polar Bear" na ni mmoja wa wanariadha mashuhuri wa Armenia wa karne ya 21.[1]