Anisia Achieng
Anisia Karlo Achieng Olworo ni Mbunge wa Sudan Kusini na mwanaharakati wa Haki za wanawake.[1]
Achieng alizaliwa Sudani kusini, mama yake alifariki akiwa mdogo na baba yake alifariki wakiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Baada ya hayo alilelewa kwenye kituo Cha kulelea watoto yatima kilichopo Uganda. Achieng alimaliiza elimu yake ya sekondari na kutaka kurudi Sudani kusini ili kutafuta ndugu zake
Achieng alikuwa akiishi katika Milima ya Nuba mwaka 1993, wakati jeshi na waasi walipoingia eneo hilo, na kumlazimisha kukimbilia Kenya ili kuhepa vita. Watoto wake wa umri wa mwaka mmoja na miaka sita walikimbilia Uganda pamoja na dada yake.[2] Huko Nairobi, Achieng alikuwa mwanzilishi mwenza wa Sauti ya Wanawake wa Sudan kwa Ajili ya Amani, shirika lisilo la kiserikali lililojitolea kupambana na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sudan.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ngunjiri, Faith Wambura (2010-02-23). Women's Spiritual Leadership in Africa: Tempered Radicals and Critical Servant Leaders (kwa Kiingereza). State University of New York Press. ISBN 978-1-4384-2978-6.
- ↑ Nebenzahl, Donna (2003). Womankind: faces of change around the world. New York: Feminist press. ISBN 978-1-55861-460-4.
- ↑ "PRESS BRIEFING BY FEDERATION OF AFRICAN WOMEN'S PEACE NETWORK, SPONSORED BY UNIFEM | Meetings Coverage and Press Releases". press.un.org. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anisia Achieng kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |