Andalio la somo
Andalio la somo (kwa Kiingereza: lesson plan) ni mpangilio au hatua zinazofuatwa na mwalimu wakati wa kufundisha somo fulani darasani. Mwalimu anapaswa kuandaa andalio la somo kabla na hata wakati wa mchakato mzima wa kufundisha.
Umuhimu wa andalio la somo
[hariri | hariri chanzo]i) Huonesha malengo ambayo mwalimu anatarajia kuyafikia katika kipindi.
ii) Humpa mwalimu mwongozo wa kufuata hatua kwa hatua wakati anafundisha darasani.
iii) Humuonesha mwalimu sehemu za somo za kuulizia maswali, kutumia zana au kuhusisha wanafunzi katika vipindi.
iv) Hutumika wakati wa mwalimu kukaguliwa na kuangalia yale aliyoyafundisha darasani na matarajio yako baada ya kufundisha.
Vipengele muhimu vya andalio la somo
[hariri | hariri chanzo]i) Jina la somo
ii) Tarehe, darasa, muda wa kipindi na idadi ya wanafunzi.
iii) Mada kuu
iv) Mada ndogo
v) Malengo ya somo
vi) Vifaa vya kufundishia na kujifunzia
vii) Vitabu vya rejea
viii) Uwasilishaji wa somo hatua kwa hatua
ix) Kazi za mwalimu na za wanafunzi
x) Maoni kuhusu mafanikio au matatizi yaliyojitokeza wakati wa kipindi
xi) Tathmini
xii) Mazoezi ya wanafunzi
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Andalio la somo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |