Aminata Touré (mwanasiasa Mjerumani)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aminata Touré

Touré in 2018

Member of the Bunge la Schleswig-Holstein
Aliingia ofisini 
29 June 2017

Vice-President of the Bunge la Schleswig-Holstein
Muda wa Utawala
28 August 2019 – 07 June 2022

tarehe ya kuzaliwa 15 Novemba 1992 (1992-11-15) (umri 31)
Neumünster, Ujerumani
utaifa Bendera ya Ujerumani Ujerumani
chama
Chama cha Kijani cha Ujerumani
Chama cha Kijani cha Ujerumani
Chama cha Kijani cha Ujerumani
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kiel
tovuti aminata-toure.de

Aminata Touré (amezaliwa 15 Novemba 1992) ni mwanasiasa Mjerumani wa chama cha Alliance '90/The Greens. Alichaguliwa tarehe 29 Juni 2017 kuwa mbunge wa kijimbo wa Schleswig-Holstein. Alikuwa kijana wa miaka 25 wakati wa uchaguzi alihudumu kama makamu wa spika wa bunge hadi 2022. [1] [2] [3] Mwaka 2022 aliteuliwa kuwa waziri wa Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Jimbo la Schleswig-Holstein.

Maisha ya mapema na elimu[hariri | hariri chanzo]

Wazazi wa Touré walikimbilia Ujerumani kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Mali ya 1991 . [4] [5] Alizaliwa 1992 huko Neumünster, Ujerumani. Mwaka 2011 alihitimu mitihani ya Abitur (Form VI ya Ujerumani) akaendelea kusoma Elimu ya Siasa na Kifaransa katika Chuo Kikuu cha Kiel hadi kupata Awali mwaka wa 2016. [6] Wakati wa masomo yake alisoma mwaka mmoja kwenye Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid. Kuanzia 2014 hadi 2017, alifanya kazi kama msaidizi katika ofisi ya mbunge Luise Amtsberg .

Kazi ya kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2012, Touré alijiunga na Vijana wa Chama cha Kijani akachaguliwa kama mwenyekiti a umoja huo mjini Kiel.

Mnamo 2016, aliingia katika kamati ya kijimbo cha chama na mwaka 2017 alichaguliwa kama mbunge wa bunge la kijimbo.

Mwaka 2019 alichaguliwa kuwa makamu wa spika wa bunge hilo.[7] Alikuwa Mjerumani Mwafrika wa kwanza na pia kijana wa kwanza kushika nafasi ya aina hii katika mabunge yote ya Ujerumani.[8]

Mwaka 2022 alirudishwa kwenye bunge la jimbo akateuliwa kuwa waziri katika serikali ya ushirikiano na chama cha CDU.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Aminata Touré". Bündnis 90/Die Grünen (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 9 July 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Grüne Touré neue Vizepräsidentin des Kieler Landtags". Retrieved on 28 August 2019. (de) 
  3. "Lebenslauf Aminata Touré". Schleswig-Holsteinischer Landtag. Iliwekwa mnamo 2022-06-22. 
  4. "Die jüngste Abgeordnete im Landtag". 
  5. "Grüne Aminata Touré über junge Politik; "Was wollt ihr, old people?"". 30 June 2019.  Check date values in: |date= (help)
  6. "Aminata Touré – Grüne Jugend SH". Grüne Jugend SH. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 July 2017. Iliwekwa mnamo 9 July 2017.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  7. "Grüne Touré neue Vizepräsidentin des Kieler Landtags", 28 August 2019. Retrieved on 28 August 2019. (de) 
  8. "Grünen-Politikerin Touré: "Ich bin nicht euer Feigenblatt"", 28 August 2019. Retrieved on 28 August 2019.