Amber Midthunder
Amber Midthunder |
---|
Amber Midthunder (amezaliwa Aprili 26, 1997)[1] ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana katika kuigiza kwenye tamthilia kama FX Legion, Roswell na New Mexico, pia alionekana katika filamu ya Longmire, Banshee, na Reservation Dogs[2][3][4]. Aliigiza kama Naru katika filamu ya Prey.[5]
Maisha ya zamani
[hariri | hariri chanzo]Mama yake Midthunder aitwaye Angelique, ana asili ya Thailand na China ni mwongozaji wa filamu[6], na baba yake David ni mwigizaji mwenye asili ya Marekani. Angelique na David walikutana wakiwa wanafanya kazi katika filamu ya Kijapani iitwayo East Meets West ya mwaka 1995.[7]
Midthunder ni raia wa Fort Peck Assiniboine na kabila la Sioux[8][9][10]. Alizaliwa katika taifa la Navajo la Shiprock, New Mexico, aliamua kurudi baada ya kutumia mda mwingi wa utoto wake huko Santa Fe ambako alihudhuria katika chuo cha Teknolojia ambapo mama yake alifanya kazi katika kampuni ya uigizaji.[11]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Midthunder akiwa mtoto alikua na shauku ya kuigiza, ambapo alikariri mistari kutoka kwenye maonyesho na filamu alizozipenda, lakini hakupenda utendaji wake wa kazi kwa mara ya kwanza na hivyo aliamua kuchukua mda kabla ya kushiriki kazi zingine[12]. Alianza kupata umaarufu katika filamu ya Sunshine Cleaning ya 2008. Midthunder aliendelea kufanya kazi katika mashirika ya uandaaji wa filamu huko New Mexico kabla ya kwenda Los Angeles akiwa na umri wa miaka 17 ili kutafuta fursa zaidi za uigizaji. Aliigiza kama Naru katika filamu ya Prey ambayo ni mfululizo wa tano katika filamu za Predator.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2021, Midthunder alipokea tuzo ya Utendaji Bora katika Tuzo za Saturn[13] na pia alichaguliwa kuwania tuzo za Critics' Choice Awards katika kipengele cha Mwigizaji bora wa kike katika filamu za Televisheni.[14]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Instagram". www.instagram.com. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Nellie Andreeva (Februari 22, 2016). "'Legion' FX Pilot Casts Amber Midthunder". Deadline (kwa American English). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ "Amber Midthunder's blossoming career with Marvel Studios". Two Row Times (kwa Kiingereza). Machi 1, 2017. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Christina Radish (Agosti 31, 2022). "Amber Midthunder on Her 'Reservation Dogs' Character and the Positive Reaction to 'Prey'". Collider (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Matt Villei (Juni 7, 2022). "'Prey' Poster Shows Amber Midthunder in the Predator's Crosshairs". Collider (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ https://nypost.com/2020/03/27/roswell-new-mexico-star-amber-midthunder-walks-us-through-season-2/
- ↑ Tripp StelnickiThe New Mexican (Februari 7, 2017). "Santa Fe actress stars on much-hyped Marvel X-Men series 'Legion'". Santa Fe New Mexican (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ "Amber Midthunder Kicks Butt as a Native Woman Superhero on FX Network's 'Legion' - Indian Country Media Network". web.archive.org. Desemba 1, 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 1, 2017. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 24, 2020. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Goddess Strides". www.natalienoel.com. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ "Post". New Mexico Entertainment (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 20, 2022. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Brian Truitt. "'Prey' breakout Amber Midthunder talks axe throwing, outwitting the Predator and representation". USA TODAY (kwa American English). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Jeremy Dick (Oktoba 21, 2022). "Prey Star Amber Midthunder Honored with Saturn Award for Breakthrough Performance". MovieWeb (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
- ↑ Kimberly Nordyke (Januari 16, 2023). "Critics Choice Awards: Full List of Winners". The Hollywood Reporter (kwa American English). Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2024.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amber Midthunder kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- Pages using the JsonConfig extension
- CS1 errors: empty unknown parameters
- CS1 errors: unsupported parameter
- Use mdy dates from November 2020
- Articles with invalid date parameter in template
- Articles which use infobox templates with no data rows
- Waliozaliwa 1997
- Watu walio hai
- Waigizaji filamu wa Marekani
- CWW24
- Mbegu za waigizaji filamu