Nenda kwa yaliyomo

Amanda Palmer (mwandishi habari)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amanda Palmer (alizaliwa 1976) anaongoza uzinduzi wa Doha Tribeca Film Festival (DTFF) na ni Mkuu wa Burudani wa Al Jazeera ya Kiingereza.

Amanda Palmer

Palmer alijiunga na DTFF kutoka Al Jazeera ya Kiingereza, ambapo kama Mkuu wa Burudani anaunda, na kutayarishwa, vipindi vya elimu na sanaa katika mtandao wa Al Jazeera. Kipindi chake cha "48" kilichochaguliwa kupata tuzo na kipindi cha "The Fabulous Picture Show," (FPS) kinachojulikana kote duniani vimemfanya ajulikane kama mtaalam wa utamaduni.

Kazi ya Palmer imesababisha watengezaji filamu wajulikane kote duniani. Kwa kujenga jukwaa la kimataifa la watengezaji filamu, Palmer amegundua talanta mpya na zinazoibukia ambayo imesababisha idadi ya wasanii wengi kupata fursa ya kuzungusha filamu zao. Katika kazi yake kwa jumla, Palmer hajawahi kusita kueleza changamoto anazopata ikiwa anarikodiwa kwa kamera au hata kazi yoyote nyingine isiyohitajiwa kurikodiwa. Baada ya kupokea shahada yake ya sanaa katika uandishi habari kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia mjini Sydney, Palmer alisomea maonyesho na muziki. Alianza kazi kama mwandishi habari wa kitaifa kwa mtandao wa Channel Seven nchini Australia kabla ya kuhamia jijini London na kuwa mwanamke mdogo zaidi kuwahi kufanya kazi kwenye stesheni iliyo Ulaya. Yeye kisha alihamia CNN na baadaye Associated Press TV kabla ya kujiunga na Al Jazeera ya Kiingereza mnamo Agosti 2005. Sasa yeye yumo katika Kamati cha Filamu Nchini Qatar.

The Fabulous Picture Show

[hariri | hariri chanzo]

The Fabulous Picture Show hutoa mtazamo mpya juu ya ulimwengu wa sinema na filamu kote duniani. Kipindi hiki hurikodiwa ndani ya sinema, ni huwakutanisha watengezaji filamu kutoka kote duniani na watazamaji. Timu ya FPS huenda kwenye sherehe za filamu zilizo kubwa zaidi kote duniani kwa mwaka wote mzima - kutoka Sundance na Berlin, Venedig, Cannes, Roma, Toronto, Marrakech, na Dubai, na nyinginezo - ili kutafuta filamu bora kte duniani. Amanda amewahi kuhojiana na watengezaji filamu na waigizaji maarufu, miongoni mwao; Martin Scorsese, Francis Ford Coppolla, George Clooney, Ang Lee, Mike Leigh, Michel Gondry, David Cronenberg, Danny Boyle, Errol Morris, Nick Broomfield, Dario Argento, Michael Winterbottom, Brad Pitt, Angelina Jolie, Halle Berry, Dennis Hopper, Russell Crowe, Joseph Fiennes, Joan Chen, Gabriel Byrne, Russell Crowe, Michelle Yeoh, Ryan Reynolds, William Dafoe, Howard Shore ambaye ni mtunzi wa Lord of the Rings na Dario Marianelli, na vilevile Gabriella Pescucci ambaye ni mshonaji maarufu aliyeshinda tuzo. FPS hutoa mkaribisho mzuri wa watengezaji filamu kutoka kote duniani ambao walioleta mabadiliko au matokeo kupitia sinema - ili watengezaji filamu wote: wapya na wanaojulikana wafaidike, na kupitia hivi huelimisha watazamaji.

Kipindi cha 48 kinahusu usafiri na utamaduni, na huonyesha Amanda na wenzake wakizunguka mahali mbalimbali kote duniani - inachunguza kila kitu kama matukio ya kitamaduni na kidini na kuzorota kiuchumi katika kila eneo, ikiwa inazingatia hadithi za watu binafsi. 48 inaangalia jinsi watu wanavyoishi maisha yao leo kama vile mashabiki wa vyuma vizito nchini Syria na 'Turbo folk' nchini Serbia; migogoro ya nyumba iliyomo Old Havana na hata majumba ya Ottoman nchini Istanbul. Mara ya kwanza, timu ya 48 ilienda Havana, nchini Cuba; Belgrad, nchini Serbia; Dameski, nchini Syria; Edinburgh, nchini Scotland; jamii ya Australia ya Ramingining; Delhi, nchini India; Accra, nchini Ghana; makambi ya wakimbizi ya Chad; Istanbul, nchini Uturuki, Marrakech, nchini Moroko; Hong Kong, nchini Uchina. Msimu wa pili mnamo Novemba 2008 ilizingatia Jiji la Ho Chi Minh, Vietnam; Buenos Aires, nchini Ajentina; Greenland; Athens, Gdansk, nchini Poland na Naples, nchini Italy.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]