Nenda kwa yaliyomo

Alkaftadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

 

Alkaftadini, yaani, Alcaftadine, inayouzwa chini ya jina la chapa Lastacaft, ni dawa inayotumika kutibu mwasho unaotokana na mzio kwenye utando unaofunika sehemu nyeupe ya jicho.[1] Inaweza kutumika kwa watu zaidi ya mwaka 1[2] na inatumika kama tone la jicho.[1] Manufaa yake hutokea ndani ya dakika 3 na yanaweza kudumu hadi masaa 16.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha macho, uwekundu, na kuhisi kujikuna.[1] Usalama wake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni kizuizi cha vipokezi cha histamini cha H 1.[1]

Alkaftadini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2010.[1] Nchini Marekani, mililita tatu ya dawa hii inagharimu takriban Dola 240 kufikia 2022.[4]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "DailyMed - LASTACAFT- alcaftadine solution/ drops". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Alcaftadine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Alcaftadine ophthalmic (Lastacaft) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Alcaftadine Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)