Nenda kwa yaliyomo

Ali Baba na Wezi Arobaini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Taswira ya hadithi ya Ali Baba, na Maxfield Parrish (1909).

Ali Baba na Wezi Arobaini ni kisa kimoja katika mkusanyiko wa hadithi katika kitabu cha Alfu Lela U Lela (Usiku Elfu na Moja).

Katika kisa hiki Ali Baba ni mkazi maskiniwa mji mmoja nchini Uajemi anayedumisha maisha yake kwa kukusanya kuni msituni na kuibeba sokoni juu ya punda zake. Siku moja anaona kundi la majambazi msituni; anajificha na kuwatazama hao majambazi wanaokaribia na kusimama mbele ya miamba mikubwa. Hapo anamsikia kiongozi wao kutamka maneno "Sesam ujifungue!" halafu uwazi kama mlango unafunguka katika mwamba, majambazi wanaingia na mlango unafungwa. Baada ya muda mlango unafunguka tena, majambizi wanatoka nje na kiongozi anatamka maneno "Sesam ujifunge!" - kumbe uwazi katika mwamba unfungwa tena.

Baada ya kuondoka kwa kundi la majambazi Ali Baba anaenda kwa sehemu alipoona uwazi na kusema maneno aliyosikia. Mlango unafunguka na Ali Baba anayeingia ndani anaona pango kubwa katika mwamba linalojaa mifuko ya dhahabu, almasi na pesa pamoja na bidhaa nyingi yenye thamani. Ali Baba anabeba kiasi cha dhahabu kwake nyumbani na kuionyesha kwa mke wake.

Kwa bahati mbaya kaka yake Ali Baba anatambua ya kwamba mdogo wake amekuwa tajiri. Akimwuliza Ali Baba anamwambia siri yake. Huyu kaka anaamua kuchukua dhahabu pia anaenda pangoni lakini wakati wa kuondoka amesahau neno lile. Anafungwa ndani ya pango hadi majambazi wanarudi wanaomwua na kuacha maiti pangoni.

Ali Baba anamtafuta kaka anapata maiti na kuichukua nyumbani kwa mazishi. Majambazi wakirudi wanatambua kuna mtu mwingine anayejua siri yao wanaenda mjini kumtafuta. Lakini Morgiana mtumwa wa kakaye Ali Baba ni binti hodari sana, anatambua majambazi na kufaulu kuwaua wote mahali wanapojificha hadi kumwua kiongozi wao kwa kisu.

Sasa Ali Baba ni tajiri. Anamshukuru Morgiana kwa kumpa uhuru na kumwoza kwa mwanawe.

Matini

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Lit-stub