Nenda kwa yaliyomo

Alex Plank

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alexander Plank

Alexander Plank (alizaliwa Juni 27, 1986) ni mtetezi wa usonji, mzalishaji wa filamu, na mwigizaji kutoka Marekani.

Anajulikana kwa kuanzisha jamii mtandaoni ya "Wrong Planet", kufanya kazi kwenye mfululizo wa televisheni wa FX "The Bridge", na kuigiza katika "The Good Doctor". Aligundulika kuwa na "Asperger syndrome" akiwa na umri wa miaka 9.

Plank alianza Wrong Planet akiwa na umri wa miaka 17, akiwa na lengo la kutafuta watu wengine wenye hali kama yake mtandaoni. Baada ya Wrong Planet kupata umaarufu, Plank alianza kutajwa mara kwa mara katika vyombo vya habari kuu katika makala zinazohusu usonji, Asperger’s, na haki za watu wenye usonji. [1]

  1. Silberman, Steve (2015). NeuroTribes: The Legacy of Autism and the Future of Neurodiversity. Avery. uk. 454. ISBN 978-1583334676.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alex Plank kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.