Adam Ro
Rashid Rauf Adam, anajulikana kama Adam Ro, ni msanii, mtunzi wa nyimbo, mwanamitindo, mwanaharakati wa kijamii, mhamasishaji nchini Ghana. Alizaliwa Ashaiman,Accra Ghana. Adam ni Mkurugenzi Mtendaji wa Adam Ro Muziki[1] [2].
Wasifu wake
[hariri | hariri chanzo]Rashid Rauf Adam alizaliwa Accra. Anaimba katika lugha yake ya asili ya Dendi na Hausa, na pia Kiingereza, Kihispania na Twi. Pia ametambuliwa kimataifa na watazamaji wa magharibi.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Adam Ro alikuwa mshiriki katika kongamano la kwanza la ACCES mwaka wa 2017 huko Dakar, Senegal. Mkutano wa ACCES unakusudiwa kuleta ushirikiano na kubadilishana mawazo kati ya wasanii wa Muziki wa Kiafrika. Adam Ro alihudhuria Kongamano la Ufikiaji wa Muziki katika Afrika nchini Kenya mwaka wa 2018. Tukio hilo ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Kitaifa wa Nairobi kuanzia tarehe 15 hadi 17 Novemba 2018 lilishuhudia baadhi ya wanamuziki bora na washikadau barani Afrika walikusanyika ili kujadili maendeleo ya muziki na sanaa katika bara hili.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Adam Ro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ https://www.pulse.com.gh/entertainment/music/new-music-adam-ro-african-story/570tzvs imewekwa mnamo 23-07-2022
- ↑ https://www.modernghana.com/music/35787/a-review-of-rising-ghanaian-international-artiste-adam-ro.html imewekwa mnamo 23-07-2022