Abemaciclib
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
N-[5-[(4-Ethyl-1-piperazinyl)methyl]-2-pyridinyl]-5-fluoro-4-[4-fluoro-2-methyl-1-(1-methylethyl)-1H-benzimidazol-6-yl]-2-pyrimidinamine | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Verzenio, Verzenios, Ramiven, Zenlistik, mengineyo |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | ? |
Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo (vidonge) |
Data ya utendakazi | |
Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 45% |
Kufunga kwa protini | 96.3% |
Nusu uhai | Masaa 18.3 |
Utoaji wa uchafu | 81% kupitia kinyesi, 3% kupitia mkojo |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | LY2835219 |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C27H32F2N8 |
|
Abemaciclib, inayouzwa chini ya majina ya chapa Verzenio miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu saratani ya matiti.[1] Hasa inatumika kwa kesi za hali ya juu ambazo ni chanya ya HR lakini HER2 hasi.[1] Inachukuliwa kwa mdomo.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara, chembechembe chache za damu nyeupe, kichefuchefu, maambukizi, uchovu, upotezaji wa nywele na chembe ndogo za damu.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha nimonia, matatizo ya ini na kuganda kwa damu.[3] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[3] Ni kizuizi cha CDK ambacho huzuia shughuli za CDK4 na CDK6.[1]
Abemaciclib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017 na Ulaya mwaka wa 2018.[3][1] Nchini Uingereza, wiki nne ziligharimu NHS takriban £2,950 kufikia mwaka wa 2021.[2] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 13,700 za Kimarekani.[4]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Verzenios". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1010. ISBN 978-0857114105.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "DailyMed - VERZENIO- abemaciclib tablet". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Verzenio Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)