Nenda kwa yaliyomo

Tanganyika Rifles : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Tanganyika Rifles''' ilikuwa jina la jeshi la Tanganyika kuanzia uhuru wa nchi mwaka 1961 hadi uasi wake na mwisho mwaka 1964. ==Historia== Tanzania bar...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:18, 27 Januari 2017

Tanganyika Rifles ilikuwa jina la jeshi la Tanganyika kuanzia uhuru wa nchi mwaka 1961 hadi uasi wake na mwisho mwaka 1964.

Historia

Tanzania bara ilipata uhuru wake kutoka ukoloni wa Kiingereza mwaka 1961 kwa jina la Tanganyika. Zanzibar bado ilikuwa nchi ya pekee. Hadi mwaka ule kulikuwa na jeshi la kikoloni katika Afrika ya Mashariki lililokuwa la askari Waafrika waliosimamiwa na maafisa Waingereza na jeshi liliitwa King's African Rifles (KAR). Vikosi viwili vya jeshi hili ambavyo askari vyao waliwahi kuajiriwa katika eneo la Tanganyika vilitengwa na KAR na kukabidhiwa kwa taifa jipya. Kikosi cha Dar es Salaam kiliitwa sasa "1st Tanganyika Rifles" na kikosi cha Tabora kilikuwa "2nd Tanganyika Rifles".

Maafisa Waingereza wa vikosi hivi waliajiriwa pia na serikali ya Tanganyika. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas.

Uasi

Katika miaka ya kwanza baada ya uhuru Waafrika wachache walipelekwa masomoni kwa vyuo vya kijeshi huko Uingereza na kupandishwa cheo kuwa afisa. Waziri wa mambo ya Nje Oscar Kambona alituma vijana wa TANU kwenda Israel kwa masomo ya kijeshi.

Kati ya askari Waafrika wa siku nyingu uchungu ulianza kuenea kwa sababu walikuwa na tumaini uhuru utaleta nafasi za kupandishwa cheo lakini waliendelea kusimamiwa na maafisa Wazungu. Pia waliona mishahara yao ilibaki kama awali ilhali Waafrika katika huduma ya serikali nje ya jeshi walipandishwa vyeo na mishahara.[1]

Katika usiku wa 19 Januari 1964 kundi la askari Waafrika walijipatia silaha wakakamata maafisa wote Wazungu na Waafrika na kusambaa mjini wakitangaza madai yao. Tarehe 20 Januari kikosi cha pili katika Tabora kiliwafuata. Maafisa Waingereza walipelekwa Kiwanja cha Ndege na kutumwa Kenya. Mawaziri wa serikali pamoja na Nyerere walijificha isipokuwa waziri Kambona alipatikana kujadiliana na waasi. Baada ya Kambona kutia sahihi na kukubali madai ya waasi Nyerere aliamua kuomba msaada wa Uingereza. Kikosi cha askari Waingereza kilifika kwa meli kutoka Aden na kumaliza uasi katika masaa machache. Kikosi cha pili huko Tabora baada ya kusikia habari hizi walitangaza ya kwamba waliacha uasi wakakabidhi silaha kwa kikundi kidogo cha Waingereza.

Hapo serikali ya Tanzania iliamua kuachisha askari wote na kumaliza Tanganyika Rifles kabisa. Jeshi jipya likaundwa katika Septemba 1964. Maafisa Waafrika waliwza kurudi na pia askari wengi wa Tabora waliajiriwa upya.

Lakini jeshi jipya liliundwa kama taasisi chini ya usimamizi raia yaani chini ya amri ya wanasiasa.

Marejeo

  1. Linganisha madai ya askari wakati wa uasi jinsi kiongozi wao Iloga alimwambia waziri Kambona, ling T. Parsons uk 111

Viungo vya Nje

Kujisomea