Kapana : Tofauti kati ya masahihisho
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Kapana ikitayarishwa '''Kapana''' ni aina ya nyama ya kuchomwa inayokatwa vipande vidogo vidogo na kuchomwa kwenye moto wa wazi n...' |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 07:54, 18 Julai 2019
Kapana ni aina ya nyama ya kuchomwa inayokatwa vipande vidogo vidogo na kuchomwa kwenye moto wa wazi nchini Namibia.[1] Mara nyingi nyama hii huuzwa kwenye soko la wazi na wafanyabiashara vijana.[2] Inaaminika kuwa biashara ya kapana husaidia kuwapatia ajira vijana[3] kwa kuwawezesha kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo.[4] Kapana ni maarufu sana katika mji mkuu wa Windhoek hasa eneo la Katutura [5].
Matayarisho
Jiko hutumia kuni huku juu ya jiko chuma imewekwa ili kuzuia nyama isianguke kwenye moto.[6]) Nyama hukatwa na panga vipande vidogo na pia huandaa pilipili, kitunguu, nyanya na prepare the chili sauce with onions, tomatoes na vikolezo vingine. Jiko linapopata moto, vipande vya nyama huweka juu ya yake. Ili kuvutia wateja, mchoma kapana huchoma kapana chache ili aonjeshe wateja, wakipenda wanachagua nyama wanayotaka ndipo anaichoma. Kapana huchomwa kwa kama dakika kumi hivi.
Utamaduni
Kapana ni njia ya kula chakula cha haraka isiyo ya gharama ya juu is inexpensive to buy and fast to cook. Sehemu inapouzwa kapana huonekana kama ni sehemu ya makutano ya kijamii ambapo watu wa aina tofauti hukusanyika.[7].
Mwaka 2014, kutokana na ukame nchini Namibia, bei ya kapana ilipanda juu.[8]
Marejeo
- ↑ "Getting Intimate with Namibia's Capital City" The Active Times
- ↑ Namibia, the land of meat lovers - CSMonitor.com
- ↑ "Creating economic space for street vendors". Development Bank of Namibia.
- ↑ "Katutura’s kapana kings". Namibian Sun.
- ↑ Sizzling kapana: Street BBQ in Namibia - CNN iReport
- ↑ "Meme Kapana take-away". Namibia Economist.
- ↑ "City fails kapana sellers". Namibian Sun.
- ↑ "Kapana scarce at Katutura Single Quarters". The Namibian.