Zama za Shaba
Mandhari
Zama za Shaba (kwa Kiingereza bronze age) kilikuwa kipindi cha historia ambacho watu walitengeneza vifaa vyao kwa kutumia metali ya shaba na baadaye bronzi yenye mchanganyiko wa metali mbili: vipande tisa vya shaba kwa kipande kimoja cha stani.
Malighafi nyingine, kama mbao na mawe, zilikuwa zikitumika pia kwa zana, lakini shaba ilikuwa nzuri zaidi kwa kukatia na kuchongea, na ilikuwa rahisi sana kuitengenezea umbo la kitu.
Zama hizo za Shaba hazikutokea wakati mmoja kila mahali, kwa sababu makundi tofauti ya watu walianza kutumia shaba kwa vipindi tofauti kabisa. Kwa mfano, Ulaya Magharibi Zama za Shaba ziliisha kunako miaka ya 2000 KK hadi 800 KK. Kumbe upande wa Mashariki ya Kati zilianza takriban miaka elfu moja nyuma.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zama za Shaba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |