Wilfred Moriasi Ombui
Wilfred Ombui Moriasi ni Mwanasiasa wa Kenya. Yeye ni Mwanachama wa Chama cha KANU. Nimbunge anayewakilisha Jimbo la Mugirango Kaskazini kwa tikiti ya Chama cha KANU[1]
Yaliyomo |
Historia[hariri]
Ombui alizaliwa katika kijiji cha Bonyunyu karibu na Kenyoro, Kata ya Itibo, Tarafa ya Ekerenyo, Wilaya ya Nyamira Mkoa wa Nyanza nchini Kenya
Elimu[hariri]
Alisoma katika Shule ya Msingi ya ELCK Kenyoro kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Kisii.
Kazi zingine[hariri]
Kando na kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi, Ombui pia anajulikana na wengi kwa kuwa meneja wa Chama cha walimu cha Mwalimu SACCOS tawi la Gusii kwa muda Mrefu.
Siasa[hariri]
Alijitosa ulingoni mwa siasa kwa mara ya kwanza wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2007. Umaarufu wake ulizambaa haraka na akakishinda kiti hicho cha Ubunge huku akiwashinda wapinzani wake akiwemo mtangulizi wake Godfrey Okeri Masanya na Mwanasheria Joseph Kiangoi Ombasa.
Tazama Pia[hariri]
| Alitanguliwa na Godfrey Masanya Okeri |
Mbunge wa Mugirango Kaskazini 2007- |
Akafuatiwa na _ |
Virejeleo[hariri]
- ↑ Members Of The 10th Parliament. Bunge la Kenya. Accessed 19 Juni 2008.
viungo vya Nje[hariri]
| Makala about a Kenyan politician bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
