Uwanja wa King Power
Mandhari
King Power ni uwanja wa mpira wa miguu huko Leicester, nchini Uingereza. Ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Leicester City F.C., mabingwa wa 2015-2016 wa Ligi Kuu. Uwanja huu ulifunguliwa mwaka 2002 na una uwezo wa kuketisha watu 32,312, ni uwanja wa soka wa 20 kwa ukubwa nchini uingereza.
Awali uwanja huu uliitwa Walkers Stadium, ulipewa jina la King Power mnamo 2011 baada ya kupata udhamini wa kampuni ya King Power.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa King Power kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |