Umandejua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Umande jua)
Umandejua
Umandejua (Drosera tokaiensis)
Umandejua (Drosera tokaiensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Core eudicots (Mimea kama alizeti)
Oda: Caryophyllales (Mimea kama fungu)
Familia: Droseraceae
Salisb.
Jenasi: Drosera
L.

Mimea ya Umandejua inaainishwa kwenye jenasi Drosera ambayo ni mojawapo ya jenasi kubwa zaidi ya mimea ambayo hula nyama. Jenasi ya Drosera ina angalau spishi 194[1]. Mimea hii ya familia ya Droseraceae huwavutia, kuwashika na kuwaua wadudu kwa kutumia viungo vyenye kuzalisha maji yenye gundi. Wadudu hawa hupendwa na umandejua kwa sababu mmea wenyewe unamea katika ardhi isiyokuwa na rotuba ya kutosha. Spishi mbalimbali, ambazo huwa na maumbo tofauti, hupatikana katika mabara yote isipokuwa Bara la Antaktiki.

Sifa za mmea[hariri | hariri chanzo]

Umandejua ni mimea inayodumu kwa miaka nyingi (lakini baadhi ya spishi hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu). Ina maua madogomadogo yaliyosimama ambayo ni karibu sm 1 na m 1 kwa urefu ikitegemea ni spishi ipi. Spishi zinazopanda huwa na shina zinazoweza kuwa ndefu sana hata kufikia mita 3, kama vile D. erythrogyne[2].

Imebainika kuwa mmea wa umandejua unaweza kuishi kwa kipindi cha hata miaka 50.[3] Jinasi hii imezoea zaidi kupata chakula kupitia kula wadudu kiasi kwamba enzaimu ya aina ya naitreti riadaktesi[4]) ambayo kawaida hutumiwa na mimea kupandishia nitrati haipo.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Maandiko ya chini[hariri | hariri chanzo]

  1. McPherson, S.R. (2010). Carnivorous Plants and their Habitats. Poole: Redfern Natural History Productions Ltd.  2 volumes.
  2. Mann, Phill (2001). The world's largest Drosera Archived 29 Septemba 2011 at the Wayback Machine.; Carnivorous Plant Newsletter, Vol 30, #3: pg 79.
  3. Barthlott et al., Karnivoren, p. 102
  4. Karlsson PS, Pate JS (1992). "Contrasting effects of supplementary feeding of insects or mineral nutrients on the growth and nitrogen and phosphorus economy of pygmy species of Drosera". Oecologia 92: 8–13. doi:10.1007/BF00317256. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Vitu vingi katika makala haya vinatoka katika tafsiri ya Kijerumani ya makala haya ya wikipedia article (retrieved 30 Aprili 2006).

  • Barthlott, Wilhelm; Porembski, Stefan; Seine, Rüdiger; Theisen, Inge: Karnivoren. Stuttgart, 2004, ISBN 3-8001-4144-2
  • Correa A., Mireya D.; Silva, Tania Regina Dos Santos: Drosera (Droseraceae), in: Flora Neotropica, Monograph 96, New York, 2005
  • Darwin, Charles: Insectivorous Plants, 1875
  • Lowrie, Allen: Carnivorous Plants of Australia, Vol. 1-3, English, Nedlands, Western Australia, 1987 - 1998
  • Lowrie, Allen: A taxonomic revision of Drosera section Stolonifera (Droseraceae) from south-west Western Australia, 2005, Nuytsia 15(3):355-393. (Online: http://science.calm.wa.gov.au/nuytsia/15/3/355-394.pdf Archived 19 Agosti 2006 at the Wayback Machine.)
  • Olberg, Günter: Sonnentau, Natur und Volk, Bd. 78, Heft 1/3, pp. 32–37, Frankfurt, 1948
  • Rivadavia, Fernando; Kondo, Katsuhiko; Kato, Masahiro und Hasebe, Mitsuyasu: Phylogeny of the sundews, Drosera (Droseraceae), based on chloroplast rbcL and nuclear 18S ribosomal DNA Sequences, American Journal of Botany. 2003;90:123-130. (Online: http://www.amjbot.org/cgi/content/full/90/1/123)
  • Seine, Rüdiger; Barthlott, Wilhelm: Some proposals on the infrageneric classification of Drosera L., Taxon 43, 583 - 589, 1994
  • Schlauer, Jan: A dichotomous key to the genus Drosera L. (Droseraceae), Carnivorous Plant Newsletter, Vol. 25 (1996)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umandejua kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.