Sirige

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sirige ni aina ya barakoa inayotumika katika ngoma za kimila za Wadogon wa Mali.

Barakoa hii inatambulika kwa urefu wake ambao unaweza kuwa kutoka mita 4 hadi 6[1].

Ina mashimo mawili zinazokwenda sambamba kutoka juu hadi chini. Pia inatumia miundo ya pembetatu kuifanya iwe maridadi. Rangi yake kuu ni nyeusi na nyeupe, lakini rangi nyingine pia zinaweza kutumika.

Mistari ya mshazari iliyo kwenye barakoa hii inaonyesha jinsi asili ya maisha duniani imeshikamana. Inavyochezeshwa mbele na nyuma huonyesha jinsi mchana na usiku hupita. Rangi nyekundu iliyo kwenye mavazi ya rapia humaanisha hedhi ya mwanamke[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "ÌMỌ̀ DÁRA". web.archive.org. 2019-07-31. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-31. Iliwekwa mnamo 2019-07-31. 
  2. Bongmba, Elias Kifon (2012-03-12). The Wiley-Blackwell Companion to African Religions (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. ISBN 9781118255544. 
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sirige kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.