Shule ya kimataifa ya Isamilo Mwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shule ya kimataifa ya Isamilo Mwanza (ilianzishwa mnamo 1956[1]), ni shule ya kimataifa ya wanafunzi wenye umri wa miaka 3 hadi 16 Mkoani Mwanza, Tanzania.[2][3] Shule hiyo imekuwa ikijulikana kama Shule ya Serikali ya Ulaya, Shule ya Msingi Isamilo na Shule ya Isamilo Mwanza kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2008 kwa jina lake la sasa.

Shule hiyo inafundisha masomo kulingana na Mitaala ya Kitaifa ya Nchini Uingereza. Shule imeongeza vidato vya tano na sita pamoja na shule ya bweni kama nyongeza kwa Hati Kuu ya Kimataifa ya Elimu ya Sekondari ambayo imetoa tangu 1998 ilipofungua shule ya sekondari.[4] Mitihani hutolewa na bodi ya Mitihani ya Kimataifa ya Cambridge.[5]

Kauli mbiu ya awali ya shule ilikuwa "Kila tabia imekamilika" na kauli mbiu mpya ya shule, iliyopitishwa mnamo 2008, ni "Mizani Sahihi". Shule imesajiliwa na Wizara ya Elimu na Utamaduni ya Tanzania (Nos: MZ.01 / 4/002 & S. 957), Idara ya watoto wa shule za Uingereza na Familia (DfCSf No. 703 6228), na Chama cha Kimataifa Shule barani Afrika.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "History of IISM". IISM (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-22. Iliwekwa mnamo 2021-06-22. 
  2. "Isamilo International School - International School". internationalschoolguide.com. Iliwekwa mnamo 2021-06-22. 
  3. "List Of International Schools In Tanzania". Tanzanian Lists (kwa en-US). 2020-09-19. Iliwekwa mnamo 2021-06-22. 
  4. "Home". IISM (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-22. Iliwekwa mnamo 2021-06-22. 
  5. https://d3giikteahxfyn.cloudfront.net/f82456c3-5769-4a9e-b8c9-a8aa4956bd4d/19a18c04-9f08-4cae-bea3-e5eaa80c8fe8
  6. "AISA Member Schools | AISA | Association of International Schools in Africa" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-06-22.