Samantha Akinyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Samantha Akinyi Okeya ( 6 Januari 1995 ) ni mtaalamu wa mpira wa miguu Kenya. Kwasasa anachezea Makalonders LFC na Harambee Starlets, Timu ya Taifa  ya mpira wa miguu ya Wanawake Kenya.

Kazi Katika Klabu[hariri | hariri chanzo]

Samantha Akinyi alijiunga na alijiunga na chama cha michezo cha vijana cha Mathare  (MYSA) mwaka 2002, ambapo alikuwa akichezea kanda ya Ruaraka Babadogo umoja wa wanawake.

Disemba 2011 alihamia chuo cha Kitaifa cha vipaji vya vijana, baadaye alijiunga ligi ya wanawake Kenya kama wasichana wa matuu na kuibuka mabingwa msimu huo, Baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Methodist cha Kenya kinachojulikana sana kama KEMU QUEENS washindi wa ligi 2015, Pia hutumia wakati Fulani na Spedag Fc hiyo ndiyo ilikuwa inatawala ligi wakati huo. Mnamo 2018 alijiunga na mabingwa watetezi Vihiga Queens Kenya.

Ligi kuu ya wanawake.[1]Ambapo aliisaidia timu hiyo kushinda ligi 2018-2019, akiibuka kipa bora wa timu mwaka huo.

Kwasasa anashiriki Makolander LFC.

Kazi Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mlinda mlango wa Kenya katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2016 dhidi ya Guinea ya Ikweta.[2] Aliwakilisha Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2016,[3] na alikuwa kipa katika mechi dhidi ya Ghana.[4][5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.the-star.co.ke/authors/connie. "Goalkeepers breath life back in Makolanders". The Star (kwa en-KE). Iliwekwa mnamo 2022-03-05. 
  2. F. K. F. Communications (2018-10-29). "AWCON 2018: Starlets set to face WPL select side in friendly". Football Kenya Federation (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-03-05. 
  3. rosewelimo (2018-02-28). "Starlets team for 2018 Africa Nations qualifiers named". KBC (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-03-05. 
  4. "Ghana 3-1 Kenya, AWCON RESULT: Suleman Samira, Elizabeth Addo, Boakye Portia strike to give Black Queens three points". Nation (kwa Kiingereza). 2020-07-04. Iliwekwa mnamo 2022-03-05. 
  5. "Ghana 3-1 Kenya, AWCON RESULT: Suleman Samira, Elizabeth Addo, Boakye Portia strike to give Black Queens three points". Nation (kwa Kiingereza). 2020-07-04. Iliwekwa mnamo 2022-03-05. 
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Samantha Akinyi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.