Robert Kisanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Robert Kisanga (20 Juni 1933[1] - 23 Januari 2018) alikuwa hakimu wa Tanzania. Alihudumu kama hakimu wa Mahakama kuu ya Tanzania na kama hakimu wa haki ya rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Alihudumu kama mwenyekiti wa kwanza katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kabla ya kustaafu mwaka 2008.

Alipata elimu katika Chuo kiku cha Birmingham (LLB) nchini Uingereza. pia alikuwa wakili ndani ya Midddle Temple katika jiji la London. Alitunukiwa Shahada ya udaktari wa heshima katika Chuo Kikuu cha Birmingham mnamo mwaka 2010.[2]

Kisanga alifariki[3] tarehe 23 Januari 2018 katika Hospitali ya Regency jiji la Dar es Salaam alipokuwa akipokea matibabu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://archives.au.int/handle/123456789/426
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-08. Iliwekwa mnamo 2023-01-24. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-02. Iliwekwa mnamo 2023-01-24.