Prison Break msimu wa 4
Prison Break Season 4 | |
---|---|
Faili:Prison-break-season-4-dvd.jpg | |
Nchi asilia | Marekani |
Mtandao | Fox |
Idadi ya sehemu | 24[1] |
Msimu uliopita | Season 3 |
Msimu wa nne na wa mwisho wa kipindi mfululizo cha televisheni cha Prison Break ulianzia kurushwa hewani nchini Marekani 1 Septemba 2008. Kipindi hiki kina sehemu 24 (22 vya televisheni na vya 2 DVD ), ambapo 16 vilionyeshwa kuanzia Septemba 2008 hadi Desemba 2008. Mfululizo wa kipindi cha televisheni ulianzishwa tena tarehe 17 Aprili 2009 na kuhitimishwa tarehe 27 Mei 2009 na sehemu mbili za mwisho. [1]
Uzalishaji
[hariri | hariri chanzo]Kulingana na TVGuide.com, rais wa Fox Kevin Reilly alielezea, "Prison Break ilifika mahali ambapo kila hadithi ilikuwa ishaelezwa." Angalau masaa sita ya maigizo yanesalia, pamoja na uwezekano wa masaa machache zaidi kuongezewa kwa vile Reilly alisema anataka kipindi "kumalizika kwa nguvu." 14 Januari 2009, Fox ilitangaza kuwa kipindi hiki mfululizo kitakuwa kinaisha msimu huu ukihitimishwa. [1]
Waigizaji
[hariri | hariri chanzo]Waigizaji nyota wa msimu wa 4 Wentworth Miller kama Michael Scofield, Dominic Purcell kama Lincoln Burrows, William Fichtner kama Alexander Mahone, Amaury Nolasco kama Fernando Sucre, Robert Knepper kama Theodore "T-Bag" Bagwell, Sarah Wayne Callies kama Sara Tancredi, Jodi Lyn O'Keefe kama Gretchen Morgan, Michael Rapaport ataigiza mara ya kwanza kama ajenti wa Homeland Security, Don Self, katika mwanzo wa msimu, wakati James Whistler (aliyechezwa na Chris Vance) na Sofia Lugo (aliyechezwa na Danay Garcia) watajitoa katika mwanzo wa kipindi-mfululizo. Kutoka sehemu kumi na moja kuendelea, Brad Bellick (aliyechezwa na Wade Williams) hayupo tena katika waigizaji.
Waigizaji wakuu wanaojirudia ni pamoja na Leon Russom kama Jenerali Jonathan Krantz, kiongozi wa Kampuni , kaimu mkuu katika kipindi ,Cress Williams kama Wyatt Mathewson, mchunguzi wa masuala ya Kampuni, James Hiroyuki Liao kama Roland Glenn, ni halifu anayewasaidia wahusika wakuu kwa mpango wao wa kuikabili na kuiteka Kampuni, Kathleen Quinlan kama Christina Rose Scofield, mamake Lincoln Burrows na Michael Scofield, Shannon Lucio kama Miriam Hultz,mpokea wageni mahala T-Bag hufanya kazi na Ron Yuan kama Feng Huan, mnunuzi wa 'Scylla', kitu muhimu sana kwa Kampuni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 Fernandez, Maria Elena. "Prison Break ending series after season", Releaselog, 14 Januari 2009. Retrieved on 14 Januari 2009. Archived from the original on 2010-04-05.