James Whistler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhusika wa Prison Break
James Whistler
Mwonekano wa kwanza: Orientación
Mwonekano wa mwisho: Scylla
Msimu: 3,4
Imechezwa na: Chris Vance
Pia anajulikana kama: McFadden
Gary Miller
Cole Pfeiffer
Kazi yake: Kachero wa zamani wa The Company
Mvuvi
Mahusiano: Sofia Lugo (demu wake wa zamani)

James Whistler (au Cole Pfeiffer, ni jina la kujifikiria ili kujiwekea utambulisho wa bandia ambao aliutumia katika mwonekano wa S04E03. "Pfeifer" ina maana ya "Whistler" kwa Kijerumani) ni jina la kutaja uhusika wa katika kipindi cha televisheni cha Kimarekani cha Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na Chris Vance. Uhusika ulitambulishwa ukiwa kama mmoja kati ya wahusika wakuu ni baada ya kufikia msimu wa tatu wa mfululizo huu.

James Whistler ni kachero wa jumuia moja kubwa ijulikanayo kama "The Company", ambaye baadaye aliswekwa lumande mjini Panama katika moja ijulikanayo kama SONA kwa kosa la kumwua mtoto wa Meya wa Panama wakati wa mapigano yao binafsi wakiwa katika baa. Huyu ndiye anayeonekana kuwa anajua suala zima la Scylla.

Na yeye ndiye alianzisha mtiti wa kutaka kuingusha The Company, akiwa pamoja kabisa na Alexander Mahone kwa msaada mkubwa wa Michael Scofield. Kwa bahati mbaya wakiwa wako uchochoroni wakizungumzia suala zima la Scylla, ghafula James akatandikwa risasi ya kichogoni na kachero mpya wa The Company na kusabisha umauti kwa James Whistler. Huyu pia alikuwa na mahusina na mwanamke wa Kipanama Bi. Sofia Lugo, vilevile Gretchen Morgan.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]