Panzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Panzi
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Caelifera (Wadudu kama panzi)
Familia: Acrididae (Panzi)
Ngazi za chini

Nusufamilia 25:

Panzi ni aina ya mdudu anayekula mimea. Panzi waainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Wanachupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Wengi wanaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa na ambao wanajikusanya kwenye makundi wanaitwa nzige.

Panzi jike wana maumbile yanayowawezesha kuchimba ardhi na kutaga mayai yao ndani ya vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya panzi aina nyingi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga) waambua ngozi zao mara tano mpaka mara saba kufuatana na aina yao. Kila hatua ya ukuaji ni kubwa kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa uambuaji wa mwisho panzi mkubwa atokea na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache.

Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Aina moja kati yao anaitwa nsenene na huliwa na watu. Jike ana umbile kama mfuo kinachofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea.

Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubisho (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula.

Picha[hariri | hariri chanzo]