Nyenje mkia-kitara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyenje mkia-upanga
Trigonidium sp.
Trigonidium sp.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Ensifera (Wadudu kama nyenje)
Familia ya juu: Grylloidea (Nyenje)
Laicharting, 1781
Familia: Trigonidiidae
Saussure, 1874
Nusufamilia: Trigonidiinae
Saussure, 1870
Ngazi za chini

Kabila 2:

Nyenje mkia-kitara (kutoka kwa King. sword-tail cricket) ni wadudu wa nusufamilia Triogonidiinae katika familia Trigonidiidae ya oda Orthoptera wanaofanana na nyenje-ardhi wadogo. Majike wana oviposito (neli ya kutagia mayai) kwa umbo la kitara na siyo upanga, kama jina la Kiingereza linavyodokeza.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nyenje hawa ni wadogo hadi wadogo sana wakiwa na urefu wa mwili wa mm 4 hadi 15 na upana wa mwili kwa ujumla si zaidi ya mm 3. Mwili wote una nywele nyingi na haswa sehemu ya juu ya kichwa na pronoto. Wana kichwa kidogo cha pembetatu na macho makubwa ikilinganishwa na ukubwa wao, ambayo kwa kawaida hujitokeza kwa mtazamo kutoka juu. Pronoto ni nyembamba kuliko kichwa. Tibia hubeba miiba. Majike wana oviposito ndefu kiasi kwa umbo la kitara. Viungo vya uzazi vya kiume ni vidogo sana na bapa na vimerefuka[1].

Kwa kawaida madume huimba au kutoa nyende (stridulation} kwa kusugua mabawa ya mbele kupitia stridulo. Mwisho huo una "kioo" kilichoendelezwa vizuri, eneo lisilo na vena.[1].

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Anacyrtoxipha albotibialis
  • Anaxipha kilimandjarica
  • Anaxipha sjostedti
  • Anaxipha vadschaggae
  • Metioche massaica

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Desutter-Grandcolas et al. (2021) Updated diagnoses for the cricket family Trigonidiidae (Insecta: Orthoptera: Grylloidea) and its subfamilies (Trigonidiinae, Nemobiinae), with a review of the fossil record. Zoologischer Anzeiger 294: 80-91.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyenje mkia-kitara kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.