Msikiti wa Umawiya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa msikiti wa Umawiya.
Kaburi la kichwa cha Yohane Mbatizaji ndani ya msikiti.

Msikiti wa Umawiya (Kiarabu: جامع بني أمية jami'a bani umaya) ni msikiti mkuu mjini Dameski katika Syria. Ni moja kati ya misikiti ya kale kabisa: ilijengwa kati ya mwaka 695 hadi 705 BK. Kabla ya ujenzi wa msikiti mahali palikuwa na kanisa la Mt. Yohane Mbatizaji lililobomolewa kwa amri ya Al-Walid aliyekuwa khalifa wa sita katika nasaba ya Waumawiya.

Mabaki ya kanisa na hekalu ndani ya msikiti[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya msikiti kuna kaburi la kichwa cha Yohane Mbatizaji kilichotunzwa hata baada ya kubomolewa kwa kanisa. Kanisa hilo liliwahi kujengwa juu ya hekalu kubwa la Jupiter na hadi leo sehemu ya kuta za nje ni zilezile za hekalu lile la kale.

Picha za msikiti[hariri | hariri chanzo]

Uwanja ndani ya msikiti umepambwa kwa picha za mosaiki zinazoonyesha miti, majani na majengo kufuatana na mtindo wa Kibizanti na wasanii walikuwa wataalamu Wakristo walioajiriwa kwa kazi hiyo. Lakini hakuna picha za watu au wanyama kulingana na kanuni za Kiislamu ingawa hata picha jinsi zilivyo hapa hazikuwekwa katika misikiti ya baadaye.

Kando ya msikiti kuna kaburi la Sultani Salah ad-Din.