Jupiter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sanamu ya Jupiter
Mkono wa sanamu ya Kiroma ya Jupiter unayoshika alama ya radi

Jupiter ni mkuu wa miungu katika dini ya Roma ya Kale. Analingana na Zeus katika dini ya Ugiriki ya Kale.

Kiasili Jupiter aliabudiwa kama mungu wa hali ya hewa aliyetawala radi na ngurumo. Baadaye alipewa nafasi ya baba wa miungu na pia wa wanadamu. Nembo yake ni radi anayoishika mkononi kwa sababu aliaminiwa ni mwenye uwezo wa kuzirusha.

Jupiter alikuwa na hekalu kubwa kabisa kwenye kilima cha Kapitoli mjini Roma penye mahekalu muhimu.

Katika utamaduni wa Kiroma sayari Mshtarii ilitazamiwa kama alama ya mungu huyu angani na sayari aliitwa kwa jina la Jupiter. Lugha nyingi za Kiulaya zinaendelea kutumia jina kwa sayari hii.



[hariri] See also

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Jupiter" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Jupiter kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.