Mradi wa Ramani ya Malaria
Mradi wa Ramani ya Malaria (kifupi: MAP) ni mradi unaokusanya habari za ugonjwa wa malaria kote duniani kwa shabaha ya kutoa ramani inayoonyesha kiwango cha hatari ya kuambukizwa kwa kila mahali.
Mradi huu unadhaminiwa kwa miaka mitano na kundi la Wellcome Trust, Uingereza [1]. Mradi wa MAP ni ushirikiano kati ya mashirika ya Afya kwa Binadamu na kundi la Epidemiologia, yaliyo kwenye kituo cha Utabibu wa Kijiografia, Kenya na shirika la Spatial Ecology na kikundi cha Epidemologia, Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Mradi wa MAP pia una vituo vya ushirikiano Marekani na eneo la Asia Pacific.
Dhamira kuu ya mradi huu wa MAP ni kubuni kadiri naganaga ya viwango tofauti vya vidudu vya malaria kama vile Plasmodium falciparum na Plasmodium vivax kwa kiwango cha Kimataifa na jinsi vinavyoenea. Jaribio la mwisho la kuchora ramani ya sehemu zinazoathiriwa na malaria ulimwenguni ilikuwa ni nyakati za 1960. Katika sehemu nyingi za dunia, hali hii bado inawakilisha ufahamu huu wa kuenea kwa ugonjwa hatari wa malaria. Mradi wa MAP wanuia kupanga, kuchora na kukadiria binadamu wanaokumbwa na hatari ya malaria ilikusaidia kubuni namna za kiustadi na za kisasa za kukadiri kwa wakati huu na wa usoni shida za ugonjwa wa malaria.
Katika sehemu ya kwanza ya mradi wa MAP, itakayoendelea hadi mwishoni mwa mwaka wa 2008, inahusisha kutafuta na kuweka rekodi ya habari na maelezo. Maelezo ya mbinu tofauti tulizotumia kukusanya maktaba kuu ya habari za uchunguzi wa idadi ya vidudu vya malaria yaani parasite rate (PR) zimenakiliwa [2]. Mradi wa MAP wakusudia kutoa kwenye Umma maelezo yote yatakayokusanywa kwenye mradi na tuliyopewa idhini ya kufanya hivyo. Toleo la kwanza kamili la maelezo ya uchunguzi wa idadi ya vidudu limepangwa kuwa mwezi wa Juni 2009 ilikuwezesha uchunguzi kamili ulimwenguni kukamilishwa na pia kuwezesha ramani zetu za ueneaji kujaribiwa na kuboreshwa.
Hivi majuzi, Mradi wa MAP ulitoa kwenye Umma ramani mpya ya uenezaji duniani ya ugonjwa wa malaria unaosababishwa na vidudu vya P. falciparum (pasipo vidudu, pale kuweko kwa vidudu kwa tegemea majira, au pale idadi ya vidudu ni imara kwani vimo licha ya majira mwakani). Hii ni sambamba na chapisho linaloelezea kinaganaga kubuniwa kwa mipaka hii ya uneaji [3]. Tafadhali tembelea tovuti ya MAP kwa maelezo na habari za kupanuliwa kwa mradi kubuni ramani za kusambaa duniani kwa mbu maalum wa Anopheles wanaosambaza malaria kwenye binadamu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hay SI, Snow RW (2006). "The Malaria Atlas Project: Developing Global Maps of Malaria Risk.". PLoS Medicine 3 (12): e473.
- ↑ Guerra CA, Hay SI, Lucioparedes LS, Gikandi P, Tatem AJ, Noor AM, Snow RW (2007). "Assembling a global database of malaria parasite prevalence for the Malaria Atlas Project.". Malaria Journal 6: 17.
- ↑ Guerra CA, Gikandi PW, Tatem AJ, Noor AM, Smith DL, Hay SI, Snow RW (2008). "The limits and intensity of Plasmodium falciparum transmission: implications for malaria control and elimination worldwide.". PLoS Medicine 5 (2): e38.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Malaria Atlas Project Ilihifadhiwa 30 Machi 2015 kwenye Wayback Machine.