Mlima wa Meza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlima wa Meza huko Cape Town
Mlima wa Meza huko

Mlima wa Meza (kwa Kiingereza: Table Mountain) ni mlima wenye sehemu ya tambarare juu na mtelemko mkali upande.

Mlima wa Meza unaojulikana zaidi ni ule wa Cape Town (Afrika Kusini), ambao urefu wake unafikia mita 1,085 juu ya usawa wa bahari. Lakini umbo hili linapatikana sehemu nyingi duniani.

Asili yake ni volkeno iliyojitokeza chini ya barafuto. Kama kutokea kwa volkeno kunaendelea bila shindikizo mno yaani bila mlipuko, basi zaha (lava) yake huyeyusha barafu ya barafuto kuwa maji. Maji yapoza zaha haraka na kusababisha umbo la pekee la mlima unaokua.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]