Mable Pinnie Koma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mable Pinnie Khutsafalo Koma (1924 - 2008) alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa mashirika ya wanawake, na mwanabiashara wa Botswana.

Alihudumu kama Mjumbe wa Baraza la Mji katika eneo la Mahalapye la Dilaene kutoka mwaka 1984 hadi 1994. Koma alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wilaya ya Kati ya Botswana kuanzia mwaka 1982 hadi 1990. Alikuwa mwanachama mwanzilishi na mwenyekiti wa tawi la wanawake la Chama cha Kidemokrasia cha Botswana (BDP) katikati ya miaka ya 70. Mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Wasichana Wakristo wa Botswana.

Maisha na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mable Pinnie Koma alizaliwa tarehe 6 Agosti 1924 jijini Mahikeng Mmamosetsanyana, Mkoa wa Kaskazini-Magharibi, wakati huo ukiitwa Bophuthatswana, Afrika Kusini. Alikuwa mtoto wa tatu kati ya kumi. Wazazi wake walikuwa Pitoro na Bela Mpa. Aliishi eneo lililofahamika kama Tlhabologo-Magogwe ambapo alikulia na wazee wake. Alikuwa akisoma katika Shule ya St Mary's (pia inajulikana kama Roma) jijini Mahikeng ambapo alimaliza masomo yake ya msingi. Kisha alihamia Holly Cross Mission jijini Alexandra, Gauteng kabla ya kwenda kusomea masomo yake ya uuguzi katika Hospitali ya Conrad jijini Taung, Vryburg ambapo pia alianza kazi yake kama muuguzi. Baada ya masomo yake, alirudi Mahikeng kufanya kazi kama muuguzi katika Kituo cha Mahikeng Clinic [1] [2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mable Pinnie Koma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.