Lynn Freed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lynn Freed ni mwandishi anayefahamika kwa kazi zake za riwaya, insha na hadithi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Lynn Freed alizaliwa na kukulia Durban, Afrika Kusini. Alienda New York akiwa mwanafunzi wa shahada ya pili akipokea shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu ya Fasihi ya kiingereza kutoka chuo kikuu cha Colombia.

Baada ya kuhamia San Francisco , aliandika riwaya yake ya kwanza Heart Change (iliyochapishwa tena kama Friends of the Family). Tokea hapo, amechapisha riwaya nyingine sita: Home Ground, The Bungalow, The Mirror, House of Women, The Servants' Quarters na The Last Laugh. Ana mkusanyiko wa hadithi fupi,The Curse of the Appropriate Man na mikusanyiko miwili ya insha: Reading, Writing & Leaving Home: Life on the Page na The Romance of Elsewhere.[onesha uthibitisho]

Hadithi fupi za Freed na insha zimetokea katika Harper's, The New Yorker, The Atlantic Monthly, Narrative Magazine, Ploughshares, Southwest Review, Michigan Quarterly Review, The Santa Monica Review, The New York Times, The Washington Post, The Wall Street Journal, Newsday, Mirabella, Elle (magazine)|Elle, House Beautiful, '[House & Garden (magazine)|House & Garden, Travel & Leisure na Vogue (magazine)|Vogue, miongoni mwa nyingine. Kazi zake zimetafsriwa kwa uwanda mpana ikijumuisha antholojia kadhaa.[onesha uthibitisho]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2002, Lynn Freed alipokea tuzo ya Hadithi za kufikirika ya Katherine Anne Porter kutoka American Academy of Arts and Letters.[1] Pia alipokea ushirika na ruzuku kutoka National Endowment for the Arts, The Guggenheim Foundation, The Camargo Foundation, The Rockefeller Foundation, na the Lannan Foundation, na the Bogliasco Foundation. Mwaka 1986, alishinda tuzo ‘the Bay Area Book Reviewers' Award for Fiction, na hadithi fupi zake zilipendekezwa kama hadithi bora Zaidi Marekani na tuzo ya "O'Henry Awards: Prize Stories".Mwaka 2011 alishinda tuzo ya O. Henry Award|PEN/O. Henry Prize kwa hadithi fupi yake ya "Sunshine," iliyochapishwa kwenye gazeti la simulizi na mwaka 2015 alishinda tena tuzo ya O. Henry Award|PEN/O. Henry Prize kwa hadithi fupi ya ,"The Way Things Are Going", iliyochapishwa kwenye gazeti la Harper's.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

  • "The Romance of Elsewhere" (2017)
  • "The Last Laugh" (2017)
  • "The Servants' Quarters" (2009)
  • "Reading, Writing & Leaving Home: Life on the Page" (2005)
  • "The Curse of the Appropriate Man, Stories" (2004)
  • "House of Women" (2002)
  • "The Mirror" (1997)
  • The Bungalow (1993)
  • Home Ground (1986)
  • Friends of the Family (first published as Heart Change, 1982)

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Archived copy". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2013-04-29.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]