Lugha ya kufundishia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lugha ya kufundishia ni lugha maalumu inayoteuliwa kutumika kutoa elimu rasmi katika taifa husika.

Baadhi ya nchi huwa na lugha zaidi ya moja za kufundishia. Kwa mfano, nchini Tanzania, elimu ya msingi na elimu ya watu wazima hutolewa kwa lugha ya Kiswahili, lakini elimu ya sekondari na ya chuo kikuu hutolewa bado kwa Kiingereza. Hata hivyo serikali ya Tanzania iko mbioni kuelekea zaidi kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia kati ngazi zote. Jitihada za kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia kina umuhimu wake katika elimu ya Watanzania ili:

1) kuifanya taaluma na elimu ya nchi kuwa na hadi ya hali ya juu.

2) kukuza maarifa ya wanafunzi

Nchini Kenya na Uganda lugha ya kufundishia ni Kiingereza isipokuWa kwa baadhi ya masomo.

Nchi ya Rwanda ilibadili lugha yake ya kufundishia kutoka Kifaransa hadi Kiingereza.

Nchi nyingi za Ulaya zinatumia lugha za nchi zao kama lugha za kufundishia.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha ya kufundishia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.