Nenda kwa yaliyomo

Kyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kyerere ni kijiji kilichoko katika kata ya Nyakatuntu.

Kijiji hiki kina vitongoji vinane ambavyo ni:

  1. Omukasamba
  2. Chijea
  3. Kyerere omusitesheni
  4. Kalebeje
  5. Chameizi(buzinza) kwaumalufu "Yerusaremu"
  6. Chitoboka
  7. Rwagati
  8. Msumbiji

Kila sehemu kuna umaarufu wake kama:

Kyerere kwa asilimia kubwa kunaishi huko koo tatu ambazo ni ukoo wa Bichechuro ukoo wa Gelumani na ukoo wa Gabriel

Kyerere ina matatizo yafuatayo:

  1. Usafiri:
  • a) barabara zote ni za udongo na hata mvua ikinyesha maji hutwama barabarani
  • b) magari machache na si imara
  1. Umeme: ni eneo ambalo halijafikiwa na umeme wa gridi ya taifa
  2. Maji: hupatikjana kwa umbali mrefu, karibia kilometa tano
  3. Zahanati: iko mbali na kijiji

Uzuri wa Kyerere:

  1. wana vyakula vya kutosha (Ndizi, maharage, mahindi n.k.)
  2. wanazalisha kahawa kwa wingi
  3. kijiji kiko karibu na Game reserve Rumanyika
  4. kijiji kiko katika ikweta yaani kijani kinaonekana mwaka mzima na hata mvua hunyesha kwa wingi
  5. Kyerere iko karibu na eneo maarufu ambalo ni: Mutata (eneo hili hutoa maji ya moto)