Kiseki
Kiseki ni lugha ya Kibantu nchini Guinea ya Ikweta na Gabon inayozungumzwa na Waseki. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiseki nchini Guinea imehesabiwa kuwa watu 11,000. Pia kuna wasemaji 3690 nchini Gabon. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiseki kiko katika kundi la B20.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kiseki kwenye Multitree
- ramani ya Kiseki
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=syi
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.