Kinyakyusa
Kinyakyusa (au Kinyekyosa; pia huitwa Kingonde au "Kimakonde") ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanyakyusa wanaokaa hasa Rungwe. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kinyakyusa imehesabiwa kuwa watu 805,000. Pia kuna wasemaji 300,000 nchini Malawi. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyakyusa kiko katika kundi la M30.
Mfumo wa Sauti (Fonolojia) [hariri]
Lugha ya Kinyakyusa ina irabu 7 na konsonanti 26. Pia, tofauti kati ya irabu fupi na irabu ndefu huleta tofauti za maana.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kinyakyusa kwenye Multitree
- ramani ya Kinyakyusa
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=nyy
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html
- http://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kinyakyusa)
Marejeo [hariri]
- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:
- Felberg, Knut. 1996. Nyakyusa-English-Swahili & English-Nyakyusa dictionary. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers. Kurasa xxii, 222. [ISBN 9976-973-32-2]
- Kishindo, J. P. 1998. IkyaNgonde: a preliminary analysis. Journal of humanities (Zomba), 13, uk.59-86.
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.