Kiazeri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Maeneo penye wasemaji wa Kiazeri

Kiazeri (pia: Kiazerbaijani, Kituruki cha Azerbaijani, kwa lugha ya wenyewe: Azərbaycanca, Azərbaycan dili) ni moja ya lugha za Kiturki ambayo ni karibu na Kituruki chenyewe.

Lugha inatumiwa katika jamhuri ya Azerbaijan na katika sehemu za magharibi-kaskazini za Uajemi, pamoja na sehemu za Georgia, Uturuki na Urusi. Idadi ya wasemaji ni takriban milioni 30.

Chanzo cha lugha kiko katika lahaja za kituruki ya magharibi zilitumiwa na wahamiaji waturuki waliofika Asia ya Magharibi tangu karne ya 10. Waturuki Waosmani walioteka Konstantinopoli waliendeleza lugha yao kama kitiruki cha Kiosmani kilichokuwa baadaye msingi wa Kituruki wa leo.

Lugha ya makabila ya Anatolia mashariki na Uajemi magharibi imeendelea kuwa asili ya Kiazeri. Wasemaji wa Kiazeri walitawala Uajemi tangu mwaka 1500 kwa nasaba ya Wasafawi. Hii ni sababu ya kwamba Kiazari kilipokea maneno mengi kutoka lugha ya Kiajemi na Kiarabu.

Tangu mwaka 1800 Urusi uliteka eneo la Kaukazi na hivyo wasemaji wa Kiazeri waliishi sasa kisehemu katika Dola la Urusi na kisehemu katika milki ya Uajemi. Kiazeri ya Kaskazini kilipokea pia maneno mmengi kutoka Kirusi.

Baada ya mapinduzi ya kirusi Azerbaijan ya Kirusi iliendelea kuwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiazeri ambako Kiazeri lifanywa lugha ya kitaifa na kukuzwa kama lugha ya kisasa. hapa maandishi ilibadilishwa kwa kutumia alfabeti ya Kikirili. Baada ya uhuru wa Azerbaijan tangu mwaka 1991 serikali ilibadilisha maandishi kuwa kwa herufi za kilatini kama vile Uturuki.

Lakini Kiazeri kinaendelea kuandikwa kwa andishi la Kiarabu nchini Uajemi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]