Kenda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kenda ni Kiswahili asilia kwa namba 9. Neno hili ni la asili ya Kibantu. Siku hizi neno "tisa" ambalo ni neno leye asili ya Kiarabu hutumiwa zaidi kutaja namba 9.

Kamusi za mwanzo na katikati ya karne ya 20 kama M-J SSE zinasema ya kwamba "kenda" iliwahi kutumiwa sawa na "tisa".

Siku hizi matumizi yake imepungua sana.

Mfano wa matumizi yake ni katika jina Mijikenda linalotaja kundi la makabila au koo 9 za Kenya.