Kanisa la Kiinjili la Armenia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kanisa la Kiinjili la Armenia (kwa Kiarmenia: Հայաստանեայց Աւետարանական Եկեղեցի) lilianzishwa na Waarmenia 40 tarehe 1 Julai 1846 huko Istanbul (Uturuki).

Lengo lao lilikuwa kusisitiza Biblia kuliko mapokeo ya Kiarmenia.

Kwa sasa kuna makanisa 88 ya namna hiyo yaliyosambaa katika nchi zifuatazo: Argentina, Armenia, Australia, Ubelgiji, Brasile, Bulgaria, Canada, Cipro, Misri, Uingereza, Ufaransa, Georgia, Ugiriki, Iran, Lebanoni, Siria, Uturuki, Uruguay na Marekani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Vahan H. Tootikian, The Armenian Evangelical Church, Armenian Heritage Committee Detroit, MI 1982
  • Rev. Hagop A. Chakmakjian, The Armenian Evangelical Church and The Armenian People