Nenda kwa yaliyomo

Kahe Magharibi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kahe)

Kahe Magharibi ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 24,466 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,142 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 25230.

Kahe ni eneo lilikutanisha jamii za kutoka Old Moshi, Arusha Chini na Milima ya Upare. Makabila yanayopatikana Kahe ni kama Wakahe, Wamasai, Wapare na Waarusha na Wameru. Aliyekuwa kiongozi wa kimila alijulikana kama Mangi Maya na badae Mangi Mangoto ambae alitawala eneo zima la Kahe. Kwa upande wa Magharibi Kahe inapakana na kiwanda maarufu cha sukari cha TPC. Hivyo baadhi ya wakazi wake wananufaika na uwekezaji huu kwa kuajiriwa kiwandani hapo.

Kahe ni maarufu mkoani Kilimanjaro kwa kilimo cha mpunga na mbogamboga kwani eneo lake lina wingi wa maji unaoruhusu kilimo kipindi chote cha mwaka. Kahe ambayo ilikuwa maarufu kwa biashara kutokana na kukutanisha reli ile inayotoka nchi jirani ya Kenya na ile inayotoka Dar es Salaam kupitia Tanga uchumi wake uliathiriwa na kufa kwa reli hiyo.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Kata za Wilaya ya Moshi Vijijini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Arusha Chini | Kahe Magharibi | Kahe Mashariki | Kibosho Kati | Kibosho Kirima | Kibosho Magharibi | Kibosho Mashariki | Kibosho Okaoni | Kilema Kaskazini | Kilema Kati | Kilema Kusini | Kimochi | Kindi | Kirua Vunjo Kusini | Kirua Vunjo Magharibi | Kirua Vunjo Mashariki | Mabogini | Makuyuni | Mamba Kaskazini | Mamba Kusini | Marangu Magharibi | Marangu Mashariki | Mbokomu | Mwika Kaskazini | Mwika Kusini | Njia Panda | Old Moshi Magharibi | Old Moshi Mashariki | Uru Kaskazini | Uru Kusini | Uru Mashariki | Uru Shimbwe


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kahe Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.