Hospitali ya Mawenzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Mawenzi ni hospitali ya wilaya mjini Moshi, katika mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Ilianzishwa mwaka 1920 kama zahanati ya kijeshi. Mnamo mwaka 1956 zahanati ya Mawenzi ilipandishwa hadhi yake na kuwa hospitali. Miaka ya 1970 hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (CMC) iliyopokea misaada mingi na hospitali ya Mawenzi ilibaki nyuma kwa kukosa misaada ya kifedha na misaada mingine.

Lakini pamoja na changamoto hizo zote hospitali ya Mawenzi bado ilibaki kuwa hospitali muhimu yenye hadhi rasmi ya hospitali ya wilaya. Hospitali ya Mawenzi ina jumla ya wafanyakazi 447, ambapo 152 ni manesi,madaktari zaidi ya 20, na wafanyakazi wengine.[1] Hospitali ina uwezo wa kutibu wagonjwa wa kutwa 300 kwa siku, na wa kulala 200. Ikiwa na vitanda 60, kwa kitanda kimoja wanaweza kulazwa wagonjwa 4. Pia hospitali ya rufaa ya mawenzi ina vitanda 40 vya kuzalishia kila siku.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mawenzi regional hospital Archived 22 Januari 2020 at the Wayback Machine., tovuti ya tanzaniavolunteers (kampuni ya kibiashara)

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]