Heli
| Heli |
|
|---|---|
| Jina la Elementi | Heli |
| Alama | He |
| Namba atomia | 2 |
| Mfululizo safu | Gesi adimu |
| Uzani atomia | 4.002602 |
| Valensi | 2 |
| Densiti | 0.1785 kg/m3 |
| Kiwango cha kuyeyuka | - K (-272.2 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 4.22 K (-268.93 °C) |
| Hali maada | gesi |
Heli (kut. kigiriki ἥλιος hélios "jua") ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 2 na uzani wa atomi 4.002602. Alama yake ni He. Ni atomi nyepesi ya pili kati ya elementi zote hivyo ina nafasi ya pili katika mfumo radidia wa elementi. Huhesabiwa kati ya gesi adimu. Heli iko katika hali ya gesi hata kama halijoto au baridi ni kali ikiganda karibu na sifuri halisi tu; ni elementi ya pekee isiyoganda kabisa hata kwenye sifuri alisi kama shindikizo ni la kawaida.
Heli inapatikana kwa wingi ni element inayopatikana kwa wingi kabisa ulimwenguni baada ya hidrojeni. Ndani ya jua letu hidrojeni huchomwa kinyuklia kuwa heli.
Muundo wa atomi [hariri]
Atomi za He hutokea kama isotopi ya He-4 yenye kiini cha protoni mbili na nyutroni mbili inayozungukwa na elektroni mbili katika ganda moja lilele.
Heli haliathiri au kuathiriwa kirahisi hivyo gesi yake haina herufu au ladha.
Matumizi [hariri]
Heli inatumiwa katika teknolojia mbalimbali hasa pale ambako baridi kali huhitajiwa kwa sababu haigandi. Tabia yake ya kutoathiriana na elementi nyingine imeifanya kuwa gesi salama kwa ajili ya chomboanga.