George Miok
George "Gyuri" Miok (18 Mei 1981 - 30 Desemba 2009) alikuwa sajenti wa Kikosi cha Ulinzi cha Kanada. Aliuawa akiwa vitani huko nchini Afghanistan mnamo 2009. Alizawadiwa nishani kadhaa na Canadian Peacekeeping Service Medal, NATO Medal for Former Yugoslavia na South-West Asia Service Medal.
Yaliyomo |
Maisha ya awali [hariri]
George (au György) alizaliwa katika familia ya Wakanada-Wahungaria mjini Edmonton, baba'ke alikuwa Illés Miok (kutoka Senta, Voivodina), mama'ke alikuwa Anna Miok (kutoka Jimbo la Veszprém), alikuwa na ndugu watatu, Michael, John na László.[1][2][3][4] Hajawahi kuoa na wala hakuwa na watoto.
Alikuwa mwalimu, alisoma katika Chuo Kikuu cha Alberta.[5] Mnamo mwaka wa 2008-2009 alifundisha masuala ya kidini, hesabu, mambo ya mazoezi kwenye jim kwa ajili ya wanafunzi wa daraja la 7 katika shule ya St. Cecilia's Junior High School mjini Edmonton.[6]
Alikuwa mwanachama wa jumuia ya Wahungaria wa Edmonton, pia alikuwa akiongea Kihungaria.[7]
Kazi ya jeshi [hariri]
Miok alijiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka 17. Mnamo mwaka wa 2002 alienda zake nchini Bosnia kutumikia kwenye Kikosi cha Udhibiti.[8] Alikwenda nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 2005. Alikuwa mwanachama wa 41 Combat Engineer Regiment na alikuwa akitumikia katika Kikosi cha Kujenga Upya cha Mkoa wa Kandahar.[9][10] Mnamo mwaka wa 2009, yeye na wanajeshi wengine watatu wa Kikanada walikufa, baada ya gari lao la silaha kupigwa na bomu la kubuni kilomita nne kutoka kusini mwa Jiji la Kandahar.[11][12][13][14] Alikuwa mwanajeshi wa 135 wa Kikanada kufa nchini Afghanistan.
Marejeo [hariri]
- ↑ DunaTV: Egész Edmonton gyászol
- ↑ George Miok wanted to teach
- ↑ Origo: Csárdás-zenekarok várják az elesett kanadai-magyar őrmestert
- ↑ Index: Magyar származású az egyik Afganisztánban megölt kanadai
- ↑ Gyászolók százai fogadták az Afganisztánban megölt kanadai katonák és újságíró koporsóját
- ↑ Edmonton school’s foyer a shrine for fallen soldier
- ↑ The Canadian Press: Grieving soldiers send remains of four slain comrades, journalist back home
- ↑ MATT pilot project
- ↑ http://www.vancouverite.com/2009/12/31/four-soldiers-named-in-kandahar-carnage/
- ↑ Global Montreal: Slain soldier Miok was torn between the army and teaching
- ↑ Gyászolók százai fogadták az Afganisztánban megölt kanadai katonák és újságíró koporsóját
- ↑ National Post: Four Canadian soldiers killed in Afghanistan identified
- ↑ HVG: Hazaszállítják a Kandahárnál megölt kanadai magyart
- ↑ The Windsor Star: Hundreds line of Highway of Heroes to honour slain soldiers, journalist
Viungo vya Nje [hariri]
- Sgt. George Miok wanted to teach
- Message of Michaëlle Jean, Governor General and Commander-in-Chief of Canada, on the occasion of the deaths of four Canadian Soldiers