Enameli ya jino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nafasi ya enameli kwenye muundo wa jino

Enameli ya jino ni sehemu ya jino inayoonekana tukifungua kinywa. Ni dutu ya ufupa mgumu sana inayofunika na kulinda kichwa cha jino au tajino.

Enameli hii inapatikana kwa meno ya binadamu na wanyama wengi pamoja na samaki kadhaa. Enameli inaweza kuharibika kwa ajali, kutafuna vitu vigumu (kama kung'ata jiwe ndani ya chakula) au kutokana na vyakula na vinjwaji vyenye sukari nyingi vinavyosababishi karisi (kuoza kwa meno).