Davido

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Davido

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa David Adedeji Adeleke
Amezaliwa Novemba 21, 1992
Miaka ya kazi 2010-sasa

David Adedeji Adeleke (anajulikana sana kwa jina la Davido; amezaliwa Novemba 21, 1992) ni mwanamuziki wa Nigeria, mwandishi na mtayarishaji wa nyimbo.

Alizaliwa Atlanta na kulelewa Lagos. Davido alianza muziki akiwa mmoja wa waimbaji katika kikundi cha muziki kijulikanacho kama (KB) International. Alisomea usimamizi wa biashara katika chuo kikuu cha Oakwood. Davido alianza kupata umaarufu pale alipotoa wimbo wake ujulikanao kama Dami Duro ambao ulikua wa pili kwenye albamu yake kutoka katika studio yake ya kwanza iliyoitwa Omo Baba Olowo mnamo mwaka 2012. Albamu hiyo ilikuwa na nyimbo sita alizozipa majina "Back When", "Ekuro", "Overseas", "All of You", "Gbon Gbon", na "Feel Alright".

Alianza muziki wake kwa kushirikisha wanamuziki wakubwa na maarufu kutoka sehemu tofautitofauti kama Nick Minaj, Young Thug, Chris Brown na Diamond Platnumz. Kupitia nyimbo hizi aliendelea kupata umaarufu wake katika tasnia ya mUziki.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Davido kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.