Campora San Giovanni
Campora San Giovanni ni kitongoji cha Amantea, Wilaya ya Cosenza, karibu na Wilaya ya Catanzaro, Italia ya kusini. Takriban wakazi 7,200 wanaishi katika kijiji hicho.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wa kijiji hicho unategemea sana kilimo na utalii. Tangu miaka ya 1950 kulikuwa na maendeleo makubwa kabisa ya ulimaji wa vitunguu vya Tropea: leo hii soko lake linakubalika ndani na hata nje ya nchi.
Miaka 20 iliyopita, ushafirishaji wa bidhaa hizi, zikiwa pamoja na biashara nyingine, umewezesha kukuza uchumi wa hapo. Maendeleo yametokana na msaada uliotolewa kijijini hapo kwa kuwapatia reli, barabara, na njia kubwa ya kupitia yenye takriban km 8 sambamba kabisa na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lamezia Terme (km 25 kutoka kijijini).
Padre wa Kanisa Katoliki wa Campora San Giovani tangu mwaka 2005 ni Apollinaris Paul Mashughuli Massawe kutoka Tanzania.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- camporaweb.it Ilihifadhiwa 12 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.