Area six

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Area six ni mtaa uliopo katika manispaa ya Morogoro, kata ya Kichangani. Zamani mtaa huu ulikuwa mmoja lakini kutokana na ukubwa wa eneo, mtaa uligawanywa na kuwa na mitaa miwili ambayo ni Area six A na Area six B.

Wakaazi wa mtaa huu inasemekana walihamia kati ya miaka 1988-1990 na hii ni kwa kuhamishwa na serikali kutoka Kichangani - Fungafunga. Uhamisho huo ulitokana na mafuriko yaliyokuwa yanasababishwa na mto Morogoro kujaa maji na kuathiri kwa kiasi kikubwa maeneo ya makazi ya watu hao.

Kabla ya jina la Area six, mtaa huo ulikuwa unajulikana kwa jina la Ninja. Asili ya neno Ninja, inasemekana lililotokana na baadhi ya matukio ya kiukabaji yaliyokuwa yanafanywa na watu kwa kipindi hicho. Ikumbukwe kwamba wakati huo eneo hilo lilikuwa ni pori kwa kiasi kikubwa, hivyo wezi au wakaji walikuwa ni wengi mno. Ulipofika wakati wa kuchagua jina ndiyo wakaita Ninja, hapa walikuwa wanamaanisha kwamba wakaazi wanaokaa hapo ni maninja. Baadaye, jina likabadilika kukaitwa Area six.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Area six kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.